Lionel Messi na rekodi zake: Mchezaji wa kwanza anayetumia guu la kushoto hat trick kwa guu la kulia

Kwa namna anavyovunja rekodi kila mara ndio maana haishangazi kuona kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuna akaunti ambazo zimefunguli...

Kwa namna anavyovunja rekodi kila mara ndio maana haishangazi kuona kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuna akaunti ambazo zimefunguliwa kwa ajili ya kuripoti takwimu zake tu.

Mchawi huyu wa kiargentina yupo katika dunia yake ya kipekee.

Akiwa ametoka kuvunja rekodi ya ufungaji bora kwenye La Liga jumamosi iliyopita kwa ha t trick dhidi ya Sevilla, Messi kwa mara nyingine tena akaivunja rekodi ya Champions League iliyowekwa na Raul katika ushindi wa Barca dhidi ya APOEL.


Usiku wa jumanne aliweka rekodi nyingi tu – inayovutia zaidi kwa kufunga hat trick yake ya kwanza kwa mguuu wa kulia – mguu ambao sio anaoutumia mara nyingi uwanjani.

*Messi ndio mchezaji wa kwanza katika historia ya michuano ya ulaya kufunga magoli na zaidi katika misimu nane mfululizo.
*Messi ndio mchezaji aliyefunga kwenye viwanja vingi (Viwanja 24) katika historia ya UCL.
*Messi ndio mchezaji aliyefunga kwenye miji mingi zaidi barani ulaya katika michuano hiyo – miji 32
*Mchezaji wa kwanza anayetumia mguu wa kushoto kufunga hat trick kwa kutumia mguu wa kulia.
*Lionel Messi ndio mchezaji aliyefunga hat tricks nyingi zaidi katika ligi ya mabingwa wa ulaya.
*Messi ndio mshambuliaji aliyefunga magoli mawili katika mechi nyingi zaidi katika UCL – (2×20)
*Wachezaji wanaongoza kwa kufunga Hat tricks kwenye UCL –
[5] MESSI
[3] Inzaghi, Luiz Adriano na Mario Gómez

*Magoli ya Lionel Messi kwa miezi:
Idadi – Mwezi
13 | September
08 | October
21 | NOVEMBER
01 | December
04 | February
13 | March
12 | April
02 | May


Related

ver 7580611678779235833

Recent

Hot in week

item