Asilimia 3.7 wanaugua kisukari ZANZIBAR
Naibu Waziri wa Afya ZANZIABR, MAHMOUD THABIT KOMBO Utafiti uliofanywa mwaka 2011 ambao umehusisha watu kati ya miaka 25 hadi 64 Kis...
https://zindukaleo.blogspot.com/2016/08/asilimia-37-wanaugua-kisukari-zanzibar.html

Naibu Waziri wa Afya ZANZIABR, MAHMOUD THABIT KOMBO
Utafiti uliofanywa mwaka 2011 ambao umehusisha watu kati ya miaka 25 hadi 64 Kisiwani ZANZIBAR umebaini kuwa asilimia 3.7 ya wananchi wa ZANZIBAR ambayo ni sawa na watu Elfu HAMSINI wanaugua ugonjwa wa kisukari.
Naibu Waziri wa Afya ZANZIABR, MAHMOUD THABIT KOMBO amesema idadi hiyo ni kubwa kwa kuzingatia udogo wa Visiwa vya ZANZIBAR ambapo idadi ya wagonjwa wapya wa Kisukari inaendelea kuongezeka na kufikia watu 300 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dokta MOHAMMED DAHOMA amesema wagonjwa wengi wa Kisukari hawafuati tiba sahihi ya kitaalamu bali kuamini tiba mbadala ambazo wakati mwingine haziwasaidii.
Mwenyekiti wa watu wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukari ZANZIBAR, WAZIRI SAID OTHMAN ameiomba serikali kuwaangalia wagonjwa kwa jicho la huruma.
