Mswada wa sheria ya dawa za kulevya kuwasilishwa bungeni

                                                       WILLIAM LUKUVI Serikali inatarajia kuwasilisha bungeni Muswada wa Sheria mpya ya ...

                                                       WILLIAM LUKUVI
Serikali inatarajia kuwasilisha bungeni Muswada wa Sheria mpya ya kudhibiti na kupambana na dawa za Kulevya katika mkutano wa bunge la 16 na 17 unaoendelea mjini DODOMA.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI amesema Sheria hiyo itaondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza wakati wa matumizi ya sheria iliyopo sasa.

Taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2013 inaonesha pamoja na mambo mengine mafanikio katika udhibiti wa dawa za kulevya katika kipindi cha mwaka 2013 ikilinganishwa na miaka iliyotangulia ambapo idadi ya watuhumiwa ilipungua kutoka 6,215 mwaka 2006 hadi watuhumiwa 1,547 mwaka 2013.

Related

Sports 6357656097803521400

Recent

Hot in week

item