Waziri mkuu kuwasilisha bungeni ripoti ya CAG

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA leo anatarajiwa kuwasilisha bungeni mjini DODOMA ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali – CAG...

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA leo anatarajiwa kuwasilisha bungeni mjini DODOMA ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali – CAG kuhusu wizi wa fedha unaodaiwa kufanywa kupitia akaunti ya kampuni ya kufua umeme nchini IPTL- TEGETA Escrow

Akitangaza uamuzi wa kamati ya uongozi ya bunge hapo jana, Mwenyekiti wa Bunge MUSSA AZZAN ZUNGU amesema licha ya kutakiwa kukabidhi ripoti hiyo ya IPTL, serikali pia kupitia kwa Waziri Mkuu imetakiwa kutoa ripoti kuhusu mauaji yaliyotokea wilayani KITETO mkoani MANYARA hivi karibuni.

Maamuzi hayo ya kamati ya uongozi ya bunge, yamekuja kufuatia miongozo iliyoombwa bungeni Mjini DODOMA na Mbunge wa KIGOMA Mjini PETER SERUKAMBA pamoja na DAVID SILINDE wa MBOZI Magharibi.
Na Katika hatua nyingine, hapo jana Bunge lilishindwa kupitisha muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa mwaka 2014 kutokana na kushindwa kukidhi akidi ya wabunge waliohitajika ili kupitisha muswada huo ambayo ni theluthi mbili ya wabunge kutoka Tanzania BARA na Tanzania ZANZIBAR.

Related

News 4889263269020529356

Post a Comment

emo-but-icon

Recent

Hot in week

item